Utamaduni Na Sanaa Za Kiafrica

By Josipha Mawakha

Utamaduni ni jinsi ya kuishi katika jamii fulani. Kuna mambo sita ya kuzingatia tukiongelea kuhusu utamaduni. Kama Mila na desturi, lugha, ishara, mila, thamani na imani.    
Utamaduni wa kiafrika ni jinsi mwafrika anavyoishi katika jamii ya kiafrika. Kuna makabila mengi ya kiafrika, mifano ni Yoruba wa Nigeria, Zulu na Xhosa wa Afrika Kusini, Wamasai wa kaskazini, kati, kusini mwa Kenya na kaskazini mwa Tanzania, Wadinka, Wanuer na Wamangbetu – Azonde wa Congo, Wabakwena na Wabangwato wa Botswana, Waembu, Wakalenji, Wakikuyu na Wakamba wa Kenya, Waovimbundu, Wambundu na Wabakongo wa Angola na Waashanti, Wafante na Waewe wa Ghana.    

Mila na desturi

Mila ni kutoa habari, imani na desturi kwa maneno au kwa mfano kutoka kizazi hadi kizazi kingine bila maelekezo yakuandikwa. Desturi ni jinsi mtu anavyo ishi katika jamii. Kuna matendo mengi ya kidesturi ambayo waafrika hufanya kama kumbusu mtu, kupiga magoti, kupeana mikono na mengineyo.
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana na zinazokubaliwa na jamii ya watu kwa mfano, kwenye bala la Africa kuna lugha nyingi sana ambazo zinazungumzwa katika nchi mbalimbali kama Kiswahili, Kiyoruba, Kihausa, Igbo, Kizulu, Kishona na nyingine nyingi.

 Itaendelea …… will be continue